Watu wengi hufikiri kuwa
computer ikiharibika inapoteza umuhimu wake. Lakini kundi la vijana kutoka chuo
cha Eden Centre kilichopo kijiji cha Nyakasimbi, Tanzania wamegundua matumizi
mbadala badala ya kutupa computer mbovu hasa Central Processing Unit (CPU).
Vijana hao
wameibalidisha C.P.U hizo zilizoharibika
kuwa kabati ya kuwekea vyombo, vyakula n.k
Issa Ismail mwanafunzi wa
chuo hicho anasema “Kabla ya ugunduzi huu tulikuwa tunatumia meza, ambayo
ilionekana kutokuwa na usalama kiusafi, tukafikiria kuwa tunaweza kutengeneza
kabati za ukutani kwa kutumia CPU mbovu zilizokuwa zimeandaliwa tayari kwenda
kutupwa”.
Mwanafunzi huyo Issa (25) wa
chuo cha kilimo na mifugo anaongeza kuwa, kwa kuwa CPU hizo zinaweza kubandikwa
ukutani hivyo kuweza kutunza vyombo vyao kwa usafi zaidi ya meza waliyokuwa wanatumia mwanzo.
No comments:
Post a Comment