NEWS

 Katika ukurasa huu tutakuwa tunakuletea habari za mara kwa mara kutoka Nyakasimbi. Na kwa maoni au maelezo zaidi, wasiliana na wataalam wetu walioko Nyakasimbi:

Yusto Nkaganyirwa- Mwandishi wa habari +255 782 427159

5 Oct. 2012

Hataimaye kijiji cha Nyakasimbi kimepata nyenzo za mawasiliano baada ya kufunga mtandao wa internet unaotumia VSAT. Haya yametokea baada ya Bw. Joseph Sekiku kukamilisha utaratibu wa malipo kupitia kampuni ya Satcom Networks iliyoko dar es salaam.

Kuwepo kwa mtambo huu, utawezesha wananchi waliokuwa wanahangaika kufuata mawasiliano kwa kusafiri mwenfo mrefu kwenda hadi kayanga takribani 47 km, kwa sasa wataweza kupata huduma hii hapa kijijini.

hata hivyo, ndugu na jama wanaoishi nje ya kijiji hiki wataweza kuwasiliana moja kwa moja na ndugu zao walioko kijijini kwa urahisi kabisa. maendeleo haya ni moja wapo ya jitihada zinazofanywa na wapenda maendeleo katika kijiji cha \nyakasimbi.

Imetimia sasa miaka 5 tangu kuanzishwa kwa huduma ya kurusha matangazo kupitia radio fadeco, hatua ambayo imesaidia pia kuitangaza wilaya ya karagwe na mkoa mzima wa Kagera.

Tutakuwa tunakuhabarisha kupitia ukurasa huu.